Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Dont Cry ft. Tupac inakuja hivi karibuni" - Chidi

4768 Chid Benz Bongo5 "Dont Cry ft. Tupac inakuja hivi karibuni" - Chidi

Mon, 8 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unakumbuka msanii wa HipHop hapa nchini Chidi Benz aliwahi kusema ana kazi zake za kumuziki na marehemu Tupac Shakur ambazo atakuja kuziachia muda ukifika.

Sasa suala hilo linaweza kutimia muda sio mrefu kwani kupitia ukurasa wake wa Instagram, amedhibitisha hilo baada ya kuandika maneno kuhusu ujio wa kazi hiyo wakati anatumbuiza kwenye jukwaa moja jijini Dar Es Salaam.

"Jana usiku, macho yote yalikuwa kwangu kama 2 Pac, amini, usiamini kila mara huwa namaanisha nachosema, "Dont cry ft 2 Pac" inakuja kwenye radio yako hivi karibuni, commando mchapa kazi" ameandika Chidi Benz

Aidha kama unamfuatilia kwenye mitandao ya kijamii utagundua kwa sasa Chidi Benz anarejea kwenye ubora wake kuanzia muonekano, mazingira na lifestyle anayoishi kwa sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live