Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dongo Janja ajitetea safari zake na mpenzi wake

Dogo Janjaro Dongo Janja ajitetea safari zake na mpenzi wake

Tue, 2 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chande ‘Dongo Janja’ amesema kusafirisafiri na mpenzi wake hakumfanyi ashindwe kuachia kazi zake za muziki.

Dogo Janja au ukipenda mwite Janjaro, amefunguka hayo katika moja ya vipindi vya Wasafi TV wikiendi iliyopita ambapo alipofafanua kuhusu kutotoa nyimbo, ndipo akaelezea kwa undani.

“Unajua safari mahusiano yangu mimi hayahusiani na muziki wangu. Mimi ninaposafiri huwa nafanya kazi ya kurekodi, nina nyimbo nyingi sana nimerekodi ambazo hazijatoka. Unajua tuna uongozi ambao unaangalia nani aachie kwa kuwa kuna msanii pia niko naye,” alisema Dogo Janja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live