Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Don Jazzy amlilia Mohbad: Hukustahili kupitia maumivu haya

Mohbad Jazzy Don Jazzy amlilia Mohbad: Hukustahili kupitia maumivu haya

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CEO wa Lebo ya Mavin Records ya nchini Nigeria, Michael Collins Ajereh maarufu kama Don Jazzy ameonesha kusikitishwa na kifo cha aliyekuwa staa wa muziki nchini humo, Ilerioluwa Oladimeji Aloba, almaarufu kama Mohbad.

Don Jazzy ameomboleza kifo cha staa huyo ambacho kimekuwa gumzo nchini humo, Afrika na maeneo mbalimbali ya dunia huku mashabiki zake wakiwa hawaelewi nini kilichompata kutokana na utata mkubwa uliogubika kuhusu chanzo cha kifo hicho.

"Inasikitisha kwamba haupo hapa kushuhudia upendo huu wote ambao ulimwengu unaonyesha. Hukustahili kupitia maumivu hayo yote. Tunakuombea Upumzike kwa Amani. Utakuwa milele katika mioyo yetu Imole," amesema Don Jazzy.

Mohbad alifariki Septemba 12 na raia wa Nigeria wametaka uchunguzi wa mwili wake ufanyike kufuatia chanzo cha kifo chake huku lebo aliyowahi kufanya nayo kazi Marlian Music kuhusishwa kwenye kifo hicho.

Baadhi ya mashabiki wa London, Uingereza, Jumatano usiku, walifanya maandamano ya kuwasha mishumaa kwa marehemu rapper wa Nigeria, Ilerioluwa Olademeji Aloba, almaarufu Mohbad.

Mashabiki hao walionekana wakiimba nyimbo za marehemu rapper katika video inayovuma kwenye mtandao. Kifo chake kilipata umaarufu wa kimataifa baada ya mashabiki kuingia kwenye mitandao ya kijamii wakitaka uchunguzi wa kina wa kufariki kwake ghafla.

SP Benjamin Hundeyin, Afisa Uhusiano wa Polisi wa Kamandi ya Polisi ya Jimbo la Lagos, amesema mwili wa marehemu Mohbad, utafukuliwa ili kusaidia uchunguzi ikiwa itahitajika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live