Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dolphin Nyembwe awaomba mashabiki kuipokea Parapanda

3794eff4 4e7e 4620 97bb C6b8c7043ca7 Dolphin Nyembwe awaomba mashabiki kuipokea Parapanda

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: mtanzania.co.tz

Texas, Marekani

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Texas, Marekani, Dolphin Nyembwe, amewaomba wapenzi wa muziki huo kusikiliza ujumbe muhimu uliopo kwenye wimbo, Parapanda.

Nyembwe, amesema katika wimbo huo alioshirikiana na Shanice Music umelenga kuwakumbusha watu kwamba Dunia ipo kwenye nyakati za mwisho na muda wowote Parapanda italia hivyo kila mmoja anapaswa kujiandaa.

“Huu ni wimbo kutoka kwenye albamu yangu ya Trumpet Parapanda ni maalumu kwa ajili ya majira haya ya siku za mwisho, muda wowote Parapanda italia hivyo kwa imani zetu tumgeukie Mungu na kumtegemea yeye peke yake, video ya Parapanda tayari ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube hivyo kila mmoja anaweza kwenda kuitazama na kubarikiwa na ujumbe huu muhimu,” amesema Nyembwe mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Chanzo: mtanzania.co.tz