Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dola Soul: Hip Hop Marekani imepoteza njia

Balozi Dola Mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva na Hip Hop Balozi Dola maarufu kwa jina la Dola Soul

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva na Hip Hop Balozi Dola maarufu kwa jina la Dola Soul ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani amesema muziki wa Hip Hop katika nchi hiyo umepoteza uhalisia wake wa mashairi yenye ujumbe wa maisha badala yake sasa wamejikita zaidi kibiashara. - Balozi aliyewahi kutamba na nyimbo nyingi amesema mabadiliko hayo pia yameathiri muziki wa Tanzania nao wamepoteza uhalisia wa muziki huo kwa kuangalia zaidi biashara badala ya kuandika ujumbe wa kubadilisha jamii kwa matukio kadha wa kadha.

“Muziki wa Hip Hop kwa sasa umebadirika mno kutokana na utandawazi na namna soko la muziki huo linavyotaka ndiyo maana wasanii wengi wanaandika mashairi mepesi yasiyo na ujumbe wa maana kwa jamii kama zamani siku hizi wamepungua mno,” alifafanua balozi.

Amesema soko la muziki kwa sasa duniani kote limebadilika lipo kibishara zaidi kuliko ujumbe ndiyo maana na Wamerakani nao wamebadilika kulingana na soko linavyotaka ingawa wamepoteza uhalisia wa muziki huo.

Ikumbukwe Balozi aliwahi kutamba na kundi la Diplomatz na kuwa kundi bora la rap nchini mwaka 1999.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live