Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dokii: Lulu Diva alichanganyikiwa na mapenzi ya Rich Mavoko

Mavoko Diva Steve Nyerere

Wed, 22 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva na Bongo Movies, Dokii amesema penzi la mdogo wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Rich Mavoko na Lulu Diva halikufa kwa sababu ya Lulu kupata bwana mwingine bali wawili hao walishindwa kuelewana kwenye baadhi ya vitu.

Dokii amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na moja ya vyombo vya habari hapa nchini baada ya kuulizwa swali kuhusu kauli ya Lulu Diva kwamba Mavoko alijitoa katika penzi hilo baada ya Lulu kupata bwana mwingine ambaye alikuwa bosi wa Mavoko.

"Lulu Diva alichanganyikiwa na Mapenzi ya Mavoko, dogo hakuwahi kuchanganyikiwa na Lulu Diva kwa sababu najua. Mavoko alitoka kwa sababu ya matatizo yao tu wao walishindwa kuelewana.

"Wanaosema Mavoko aliondoka kwenye penzi na Lulu Diva sababu ya bosi wake sijui Diamond hayo ni maoni yao. Mimi najua sababu ni nini n ahata Lulu Diva mwenyewe anajua. Lulu Diva ndio alichanganyikiwa na penzi la Mavoko, hilo nasema ukweli," amesema Dokii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live