Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dogo aliyemtesa bilionea Elon Musk atua Threads

Elon Musk Dogoosz Dogo aliyemtesa bilionea Elon Musk atua Threads

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nilipoamka asubuhi ya Desemba 14, 2022 nakutazama simu yangu nilikutana na jumbe nyingi kutoka kwa marafiki zikinifahamisha kuwa account yangu ambayo ilikuwa ikifuatilia ndege ya Elon Musk imefungiwa alisema Jack Sweeney Jack Sweeney ni nani?

Ni kijana kutokea nchini Marekani ambaye umri wake unakadiriwa kuwa ni kati ya miaka 20 - 21, Jack amejizolea umaarufu kuanzia miaka ya 2020 kwa uwezo wake kwenye kuipambanua teknolojia haswa upande wa anga.

Baba wa Jack ni Technical Operator ndani ya kampuni ya ndege inayofahamika kama American Airlines na ndiye aliyesababu kwa jack kusomea Programming pale chuo kikuu cha central florida kwani alimpa elimu kuhusu mambo ya anga angali bado mdogo.

Kwa nini alifahamika kwa umma? Uwezo wake kwenye kufuatilia mawasiliano ya ndege za watu mashuhuri na kuweka mtandaoni ndio kitu kilimpa umaarufu mkubwa mitandaoni, Mwaka 2022 alifahamika zaidi baada ya kutengeneza account kwenye mtandao wa Twitter ilifahamika kama ElonMusk's Jet.

Account ambayo ilikuwa mahususi kwenye mtandao huo kwa lengo la kufuatilia safari za ndege za Billionea Elon Musk, Jambo ambalo kiusalama kwa tajiri kama Elon ni hatari hivyo alipewa machaguo kadhaa ikiwemo vitita vya pesa ili kusitisha lakini alikaidi mpaka pale account yake binafsi na hii ya kufuatilia mawasiliano wa Elon Musk kufutwa kwenye mtandao wa Twitter.

Kwa nini Tunamzungumza hapa kwa sasa? Ni kwa sababu amerejea tena baada ya kufutiwa account zake kwenye mtandao wa Twitter, Na sasa baada ya kutambulishwa kwa mtandao wa Threads amekuwa ni mmoja wa waliojiunga kwenye mtandao huo, huku akiwa anaendeleza kazi yake ya kufuatilia mawasiliano ya Bilionea Elon Musk.

Kwenye mtandao wa Threads kwa sasa ana wafuasi zaidi Elfu 79, bado haijafahamika hatua gani zitachukuliwa kutokea hapo ukizinga mtandao wa huu unamilikiwa na mshindani wake wa kibiashara ndugu Mark, hii inaweza kuchukuliwa kama nafasi ya kumfifisha Elon kwa namna moja au nyingine kwani suala la usalama kwake unaweza kuwa mdogo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live