Msanii wa Chuga Chugani anayedaiwa kuwa na miguu ya mapenzi aitwaye Dogo Janja maarufu kama Janjaro, ameweka wazi kuwa mpaka leo mrebo wa Bongo, Irene Uwoya, anamuelewa sana kiasi cha kuwa anachati naye mpaka sasa.
Dogo Janja amefichua siri kuwa kilichomfanya Uwoya amkumbuke mpaka sasa, ni mapenzi aliyokuwa anampatia ambayo anadhani hakuna mwanaume yeyote aliyewahi kumpa mapenzi hayo.
Akizungumza kuhusu kurudiana na mrembo huyo ambaye waliwahi kufunga ndoa na kuishi pamoja kama mke na mume, Dogo janja amesema kwa sasa yupo kwenye mahusiano hivyo itakuwa ngumu kurudi kwa Uwoya.
Unadhani Uwoya alipewa nini?