Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dogo Janja: Sina mawasiliano na Uwoya

Uwoya Pic Data Dogo Janja: Sina mawasiliano na Uwoya

Tue, 2 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Janjaro kutoka Arusha, Dogo Janja amesema kwamba kwa sasa yeye na muigizaji Irene Uwoya imebaki story tu, hawana mawasiliano hata ya kuibia.

Dogo Janja amezungumza hayo juzikati alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi TV ambapo watangazaji wa kituo hicho walitaka kujua juu ya taarifa za kwamba Uwoya amekuwa akimpigia sana simu bwa’mdogo huyo ambaye anafanya muziki wa Hip Hop.

“X yupi unazungumzia maana mimi nina ma-X wengi?” alihoji Dogo Janja na kujibiwa kuwa ni Uwoya.

“Uwoya hatuna mawasiliano yoyote mimi na yeye. Tumesha-move on na sisi ni watu wazima, yeye ni mtu mzima na mimi ni mtu mzima,” alisema Janjaro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live