Filamu ya hali halisi (Documentary)ya ziara ya dunia ya Renaissance ya Beyoncé itatolewa katika kumbi za sinema mnamo Desemba 1, AMC Theatres ilitangaza Jumatatu.
Tiketi za filamu hiyo zitaanza kutoka $22, huku mwimbaji akiripotiwa kupokea angalau 50% ya mauzo ya tiketi.
Makala hii inaangazia ziara ya miji 39 ya Renaissance ambayo ndiyo imekamilika baada ya kuipambania kwa miezi mitano kuanzia Stockholm, Uswidi na kuishia Kansas City, Marekani.
Ziara hiyo, iliyofuata albamu yake iliyoshinda Grammy ya 2022 ya Renaissance, inachanganya picha za tamasha na vipengele vya taswira wakati wa kufuatilia ziara hiyo.
Katika kipindi cha miezi mitano, karibu washiriki wa tamasha milioni 2.7 walihudhuria na ziara hiyo iliyoingiza karibu dola milioni 500, kulingana na Billboard.
“Ni kuhusu nia ya Beyoncé, bidii, ushiriki katika kila kipengele cha utengenezaji, akili yake ya ubunifu na madhumuni ya kuunda urithi wake, na ujuzi wa ufundi wake,” yanasomeka maelezo ya filamu hiyo.
Filamu za awali za msanii huyo ni pamoja na filamu ya 2019 ya Netflix Homecoming, iliyolenga Coachella performance ya mnamo mwaka 2018.