Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Mwakaje ateuliwa kuwa mwenyekiti BASATA

Saudin Jacob Mwakaje Dkt. Mwakaje ateuliwa kuwa mwenyekiti BASATA

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Saudin Jacob Mwakaje kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Dkt. Mwakaje ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mjumbe wa Baraza lililomaliza muda wake.

Rais Samia amemteua pia George Nathaniel Mandepo kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania akichukua nafasi ya Griffin Venance Mwakapeje ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kabla ya uteuzi huu Mandepo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usuluhishi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Amemteua pia George Daniel Yambesi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) kwa kipindi cha pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live