Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Kumbuka asimulia alivyougua kichaa miaka 3

DK KUMBUKA Dk Kumbuka asimulia alivyougua kichaa miaka 3

Thu, 7 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Salehe Nassoro ‘Dk Kumbuka’ ameeleza mapito yake aliyopitia ikiwemo suala la kuugua kichaa kimazingara.

Dk Kumbuka amesema, akiwa tayari ni maarufu, alirogwa na watu wasiopenda maendeleo yake na kujikuta akiugua kichaa kwa takriban miaka mitatu.

“Namshukuru Mungu, ndugu zangu walipambana, lilikuwa ni jambo la kifamilia na hakuna ambaye aliweza kujua Dk Kumbuka yupo wapi.

“Mimi siamini ushirikina lakini kwa niliyopitia unaona kabisa ni hayo mambo maana sikuwa na tatizo la akili wala nini lakini ghafla tu nilianza kupiga makele,” alisema Dk Kumbuka.

Kwenye mahojiano hayo aliyoyafanya na Global TV Online, Kumbuka pia aligusia suala la zawadi ya gari aliyomnunulia mkewe hivi karibuni kwa kusema alifanya hivyo kwa sababu wametoka mbali.

“Watu hawajui, mimi na mke wangu hatukukutana ukubwani. Ni family friend, mke wangu anaenda shule mimi namuona hivyo nilipanga tu kwamba Mungu akinijalia nimnunulie gari mke wangu,” alisema Dk Kumbuka.

Dk Kumbuka alisema, mkewe huyo amemvumilia mengi likiwemo suala la kuambiwa kuwa yeye ni mwanaume ambaye siyo rijali jambo na wameweza kudumu kwa takriban miaka 10 ndani ya ndoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live