Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diva aeleza alivyokuwa akimlea Heri Muziki (+Video)

Mon, 29 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm, Diva ameeleza alivyokuwa akimlea aliyekuwa mpenzi wake Heri Muziki.



Akiongea na Bongo5, mrembo huyo pia amebaisha kuwa ngoma ya ‘Waambie’ ni ngoma yake ila alimpatia nafasi Heri kama msanii.

“Guys tuanzia hapo mwaka 2017 mwishoni niamua kufanya vitu wanavyofanya watu kama Major Lazer, Allan Walker na producer wengine kama Dj Khaled wanakuwa wanampa mtu kazi lakini ngoma ni ya kwake,” ameeleza mrembo huyo.

Akaongeza “Niliamua kufanya hii albamu ku-support wasanii wa RnB ambao wanataka kutoka lakini kutokana na muziki wa Tanzania unavyokuwa inakuwa ngumu kwa msanii wa RnB kutoka, labda abadilike aende kwenye Bongo Flava. So nikakaa chini mimi na producer wangu nikamwambia nataka nifanye hii albamu kwa sababu 1,2,3,4,5 so nachotakiwa sasa hivi ni kuangalia watu wenye uwezo mkubwa na kuwashirikisha tuka wasaliana na wasanii wa Hip Hop pamoja na wasanii wa nje ya nchi. Katika majadiliano na mtayaraishaji tuka waza nani anafaa tukaona ni Nandy but Nandy alikuwa busy vocation, ila wakatuahidi kuwa atakuwepo and i hope yupo katika albamu wakati namsubiria ndiyo ikaja idea ya huyo mtu ambaye watu wanadai ni ngoma yake lakini hapana.”

“Nilichofanya mimi kumpigia na kumwambia hey kuna hiki na hiki akaniambia am Okay with it, nikamuuliza unataka nikulipe akasema No nachotaka nionekane nimefanya kazi yako na ngoma yako. Hata hizi interview nyingi ukisikiliza anasema kuwa ngoma ni ya Diva so nilikaa na mwanasheria wangu maana tulijua kuna some problem zita occurs tunakakaa chini tuka msainisha Producer ngoma kisheria na tukaenda COSOTA kuisajirisha hii nyimbo ambayo ipo chini yangu, COSOTA wataandika barua this very soon kumstopisha na kuacha kuendelea kutumia kazi ambayo sio yake,” amedai mrembo huyo.

Akasisitiza “Kwa Watanzania ambao hawaelewi wanaanza kushangaa hii nyimbo kaimba fulani then Diva anaimba, lakini hapana nyimbo ni yangu nimelipia kila kitu nime organize Tommy Flavour, nimelipa studio nimetumia kama milioni mbili maana huyo mtu aliyekuwa ameingiza vocal tumemtoa. Ila alipokuwa akienda studio nilikuwa na hakikisha nampa elfu hamsini au sabini kila alipokuwa anaenda studio, photoshoot nimempa laki tano na vitu vitu vingine, simu ya Iphone nimempa for promotion so yo see nilijitoa sana for this project nilivyoona inaaza kuharibika nililaumiwa sana na mabosi zangu.”

Chanzo: bongo5.com