Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diva aapa kumburuza Gigy mahakamani

Gigy Na Diva Diva aapa kumburuza Gigy mahakamani

Sun, 2 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ohooo! Jambo limezua jambo. Baada ya Gigy kueleza chanzo cha ugomvi wake na mtangazaji Diva, mtangazaji huyo ameibuka na kusema anamburuza mahakamani.

Diva amesema, Gigy anazusha maneno machafu kumhusu yeye jambo ambalo limemsababishie dili lake la milioni hamsini hivyo amezungumza na mwanasheria wake kwa ajili ya hatua za kisheria.

“Nimewaambia hata watu waliopandisha baadhi ya interview pale Wasafi waziondoe. Halafu sijui ananionaje mimi nina kesi yake polisi kwanza na sijawahi kuifuta, namsikia anaongea ujinga sasa acha twende kisheria,” alisema.

Gigy amefanyiwa mahojiano hivi karibuni ambapo alimtuhumu Diva kuwapa nafasi kina Niffer na Nai kumsema vibaya redioni kufuatia kauli yake ya kuwakosoa baadhi ya mabinti wanaomiliki maduka mjini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live