Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diva: Ndoa tamu, raha zilezile

Diva: Ndoa Tamu, Raha Zilezile Diva The Bawse

Wed, 8 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa kituo cha Radio cha Wasafi, Diva The Bawse amefunguka baada ya watu kuanza kumsakama mitandaoni kisa kuhama Magomeni alikokuwa akiishi na mumewe, Abdul.

Diva kupitia mtandao wa Instagram amesema; “Jana kuna habari zilienea kwa kasi sana kwamba mimi na mume wangu Abdul tumeachana kisa nimehama Magomeni, kwan magomeni hawaishi watu, mbona watu wa Magomeni wakarimu tu sana yani.

“Sema y'all know me, kuishi Mikocheni, Masaki, Mbezi beach really affected me, is a lifestyle. So guess Magomeni not for me but love y'all watu wangu wa Migo nimekaa mwezi tu nime enjoy sana misosiii kuna mzee na mke wake wanapika chapatti harage nyie kelele moja kwao.

“Ni kweli kabisa sio nimehama tumehama wote ila kuna kitu kizuri kinakuja so mtafurahia. Abdul is hard working, anajitajidi kama mume ingawa wenyewe mnajua ninavyopenda, raha na yes anajitajid mtoto wa watu.

“Ila bado tutakuwa available Magomeni weekdays, mchana muda wa kazi au sio? So wenye sijui barua kuniandikia, wenye kutaka kuonana na mimi kikazi Magomeni will be a new location kwa mchana.

“Reason ya kuhama ni sababu nahitaji kukaa karibu na ofisi, Mbezi ninapoishi na Wasafi ni pua na mdomo dakika 5 tu, ndiyo maana nikaingia Insta-live muone.

“Stori za kuachana nani kwanza alianzisha?! Caption zangu huwa ni for my podcast link in my bio mimi ni mutu ya habari, ila ni love expert, ila pia ni star, so msiwe mnachanganya sana mambo mtapasuka mioyo yenu, nitawachanganya!

“Last thanks to our fans msijali si tupo bwana raha zilezile, ndoa tamu! good morning @sheikh_abdulrazak_salum ,” ameandika Diva Thee Bawse.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live