Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diva: Nashambuliwa sana kisa ndoa, nimechoka

DIVA THE BAWSE Diva: Nashambuliwa sana kisa ndoa, nimechoka

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diva The Bawse; ni mtangazaji wa Wasafi ambaye amekiri kupitia changamoto kubwa kwenye ndoa yake.

Diva anasema kuwa, changamoto kubwa anayokutana nayo kwa sasa kwenye ndoa yake ni pamoja na kushambuliwa kwa maneno makali, kisa mumewe, Abdurazak, lakini kesi nyingi ni za wanawake.

Anasema; “Kesi za wanawake nyingi nimechoka eti, nilifikiri ndoa mtu akiwa mke anaheshimika, lakini ndoa yangu inakuwa ya kushambuliwa na wanawake kila kukicha, kulala walale wao, matusi kwangu inahusu?

“Sielewi mpaka dakika hii kwa nini wananiingiza katika ujinga wao so ule upole kwangu saa hii sina, naona heshima eti niliolewa kwa heshima sikuokotwa, mi’ ni mke halali mpaka tukishindwana labda na kama kuna mtu alikuwa naye huko siyajui sielewi why wananikosea heshima kiasi hiki…”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live