Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diva: Nalipwa Mil. 10 kwa mwezi

Diva Safi Diva: Nalipwa Mil. 10 kwa mwezi

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji Diva The Bawse amesema, kama asipotumia kwa fujo hela zake anazolipwa kama mshahara basi kwa mwezi anakunja si chini ya milioni kumi.

Diva ameyasema hayo mapema leo alipokuwa anafanya mahojiano na Global TV Online ambapo alizungumzia mapito yake hadi kuwa mtangazaji maarufu Bongo.

Diva alisema, kwenye safari yake hakuwahi kufikiria kufanya kazi ya utangazaji lakini ilitokea baada ya kumpeleka rafiki yake Clouds kupeleka barua ya field na ndipo alipoanza kujifunza na baadaye akawa mtangazaji mashuhuri.

Kuhusu mshahara anaolipwa kwa sasa Wasafi FM, Diva alisema anakunja fedha hizo na kwamba anamshukuru Diamond kwani alimwezesha kwa kila alichokihitaji tangu alipojiunga na redio hiyo.

“Nisipofanyafanhya hizi shopping, kwa mwezi naweza kuweka ndani milioni kumi na hizo ni za mshahara tu, bado matangazo yangu Instagram,” alisema Diva.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live