Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Director Kenny aanika sababu Bongo kutotumika kwenye shooting

Director Kenny Ers Director Kenny

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwongozaji mahiri wa video za wasanii wa Bongo, Director Kenny amefunguka sababu za wasanii wa Marekani kutokuja Bongo ku-shoot video na badala yake kwenda nchi kama Uganda.

“Vidieo ni scene na scene, inategemeana mtu anataka apate nini kwenye kitu flani, kwa hiyo unakuta kwenye scene yake Tanzania hajaiweka kichwani, au anaona ni mbali wakati mwingine hatujitangazi vizuri.

“Watu wanakwenda mfano Misri kwa sababu wanataka kuyaona ma-pyramids. Wanakwenda Uganda kwa sababu wanaweza kuona Uafrika wa kweli, ndiyo maana wengi wanakimbilia kule.

“Kama mtu anakuja Afrika kuna kitu atakihitaji, labda kwenye scene yake anataka Bahari au Uafrika zaidi. Tanzania sio watu wa culture, sisi tumeiga sana huko nje, hatuna utamaduni wetu ambao unatutambulisha moja kwa moja,” amesema Kenny.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live