Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Director James Cameron wa Titanic kuhusu kuandaa filamu ya OceanGate

James Cameron Director James Cameron.

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Director wa filamu ya 'Titanic' James Cameron, amekanusha uvumi kwamba anatayarisha filamu kuhusu 'OceanGate Submarine' iliyopata hitilafu na kusababisha vifo vya watu watano, 18 June 2023.

Jame Cameron ambaye ni mtaalamu wa muda mrefu kwenye safari za chini ya maji za kwenda kutazama mabaki ya Titanic amesema 'Sipendi kujibu uvumi unaokera kwenye vyombo vya habari kwa kawaida, lakini nahitaji sasa kusema, SIPO kwenye mazungumzo kuhusu filamu ya OceanGate, wala sitawahi kufanya filamu hio".

Baada ya kauli hii, comment kwenye blogs nchini Marekani zinataka James atengeneze filamu hii ili watu waone jinsi tukio hilo lilivyokuwa kwani wanaimani kuna mambo yamefichwa na vyombo vya habari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live