Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dimpoz kupostiwa na Man United ni 'U-Freemason' - Mwijaku

Ommy Mwijakuu Dimpoz na Mwijaku

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu Bongo, Ommy Dimpoz yupo nchini Uingereza ikiwa ni wiki sasa kwa mwaliko rasmi wa timu ya soka ya Manchester United na amekuwa akiposti picha alizopiga na wachezaji mbali mbali wakiwepo wa timu hiyo na wale wa Liverpool baada ya kukutana nao katika mechi ya EPL usiku wa Jumatatu wiki iliyopita.

Tukio lililozungumziwa zaidi ni baada ya ukurasa rasmi wa Instagram wa timu ya Manchester United kuiposti picha ya Ommy kwenye instastories zake na hili limekuwa gumzo haswa nchini Tanzania, baadhi wakisema kwamba msanii huyo ametumia ‘uchawi’ mpaka kutambuliwa na ulimwengu mzima wa mashabiki wapatao milioni 59.9 wanaoshabikia timu hiyo kwenye Instagram.

Mmoja wa watu ambao wametilia shaka uswahiba kati ya Dimpoz na Manchester ni mtangazaji mwenye Mwijaku ambaye ameibuka na suala la ushirikina ambao Watanzania wengi wanaliita "U-freemason" na kusema kwamba haiwezekani kwa Ommy kukwea mpaka kujipata kwenye ukurasa wa timu kubwa hivo pasi na jambo la ulozi ambalo limetumika.

"Kuna siri gani kati ya Man United na @ommydimpoz. Mpaka kwenye ukurasa wao jamani? Au freemason? Haiwezekani," aliandika Mwijaku katika ukurasa wake wa Twitter.

Mtangazaji huyo pia alizidi kukanusha ukweli na uhalisia huo wa Ommy kupakiwa kwenye Instagram ya Manchester United na kuzidi kulalama kupitia kurasa mbali mbali za mitandao yake ya kijamii akisema kwamba huenda kama si ushirikina basi kuna tajiri mwenye ushawishi mkubwa sana nyuma ya ziara ya Ommy kule katika jiji la Manchester.

"Haiwezekani..! Jamani kuna siri gani hapa? @ommydimpoz huyu huyu au kuna TAJIRI nyuma yake? Natamani nimjue..!" Mwijaku alilia.

Imekuwa ni kawaida sana kwa Wabongo kutuhumu wenzao wamejiunga kwenye Ufreemason mara baada ya Mafanikio ya ghafla, hivyo sio ajabu kabisa Mwijaku kumtuhumu Ommy Dimpoz.

Mpaka sasa inadaiwa kuwa Ommy Dimpoz anatamba kuwa ndio Mtanzania wa kwanza kupiga picha na Cristiano Ronaldo pia ndio Mtanzania wa kwanza kupostiwa kwenye page ya Manchester United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live