Mbali na kwamba Ommy Dimpoz kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ubunifu wa kampuni ya GSM, ni bosi haswa lakini hajawasahau Mashabiki zake wanaoupenda Muziki wake.
Sasa Good News ni kwamba mkali huyo ametangaza ujio wa Album yake mpya aliyoipa jina la Dedication yenye nyimbo 15 ambayo anatarajia kuiachia Mwezi Novemba tarehe 4 Mwaka huu.
Staa huyo aliwajuza mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa instagram kuhusiana na ujio wa album hiyo na kuandika…
“LADIES & GENTLEMEN kwanza Napenda kuchukua nafasi hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu Kwa Afya na Uzima Alhamdulilah pili kwa Furaha ya Kipekee Tarehe 4 November 2022 siku ya Ijumaa panapo uzima Naenda kuandika historia mpya katika Maisha yangu kwani Album Yangu Ya kwanza toka nianze Muziki itatoka Rasmi jina la Album ni DEDICATION.
"Haikuwa Kazi Rahisi Ukizingatia Mapito niliyopitia Lakini kila kitu kina Muda wake. Shukrani za Dhati Kwa Watu Wote Ambao Wamesaidia mimi kufika hapa Kuanzia Team yangu, Familia, Marafiki na Wadau MbaliMbali Ambao kila mmoja ana mchango hata kama ni mdogo katika Maisha yangu kwa Ujumla Asanteni sana”- Ommy Dimpoz