Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dimpoz atamba kuwa ndio Mtanzania wa kwanza kupiga picha na Ronaldo

Ronaldo Dimpoz Dimpoz na Ronaldo na Fred

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' ametamba baada ya kupiga picha na wachezaji maarufu wa timu ya Manchester United ya nchini Uingereza.



Dimpoz ambaye anatajwa kuwa mtu wa bata kama lote, ame-post picha katika ukurasa wake wa Instagram alizopiga na Wachezaji wa timu ya Man United akiwemo Cristiano Ronaldo baada ya mechi ya jana ya Manchester United Vs Liverpool ambao Manchester alishinda kwa bao 2-1.



Dimpoz hajaishia kuposti tu, staa huyo ambaye ni shabiki waan United na Klabu ya Simba, ameposti picha hizo na kudai kuwa yeye ndiya amekuwa Mtanzania wa kwanza kupiga picha na mchezaji maarufu wa nje Cristiano Ronaldo.

Dimpoz ameandika kuwa; “Mimi ndo mtanzania wa kwanza kualikwa rasmi na Klabu ya Manchester United na ni Mtanzania wa kwanza kupiga picha na Cristiano Ronaldo na wachezaji wote kama yupo wa kubisha aje hapa,” amesema Ommy Dimpoz.

Mbali na Ronaldo, Dimpoz amepiga picha na Jadon Sancho ambaye ndiye mfungaji wa bao la kwanza la Man United jana, Fredy ambaye aliingia pamoja na Ronaldo kipindi cha pili dakika za mwisho, Tyrell Malacia na Cristian Eriksen.



Una maoni yoyote? Endelea kutembelea #TanzaniaWeb.com

Chanzo: www.tanzaniaweb.live