Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dimpoz asimulia alivyochongewa afukuzwe kazi GSM

Dimpoz Asimulia Alivyochongewa Afukuzwe Kazi GSM.jpeg Dimpoz asimulia alivyochongewa afukuzwe kazi GSM

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Fleva Omari Nyembo 'Ommy Dimpoz' amesimulia jinsi watu walivyomchongea ili apigwe chini na kampuni ya GSM ambayo imemuajiri.

Dimpoz ametoa inshu hiyo alipokuwa akmtakia heri ya kuzaliwa big boss wa GSM, Ghalib Saidi Mohamed.

"Uzuri wa tajiri yangu hana kifua friji haligandishi. Siku moja aliniambia unajua watu wanakupiga sana majungu kuna mmoja kaniambia vipi unampa kitengo Ommy hajasoma wakati watu tuna PHD lakini Allaah amemjaalia hekima akamjibu mimi siangalii makaratasi kama mtu nikimpa majukumu na akayafanya vyema sina neno.

"Nakuombea kwa Mungu kaka yangu wewe ni mtu mwema sana hakuna binadamu aliyekosa mapungufu lakini Allaah amekujaalia roho safi na ishaallaah, endelea kutushika mkono sisi wa chini tuendelee kutimiza ndoto zetu HAPPY BIRTHDAY SIMBA GSM" aliandika Dimpoz kwenye ukurasa wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live