Msanii wa Bongo Fleva, Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' amefunguka kuhusu kumaliza tofauti zake na msanii mwenzake Diamond Platnumz ambapo amesema kwamba ilikuwa ni utoto na kwasasa haina maana tena kuendelea kuwa na utofauti.
Dimpoz amesema maisha ya sasa huwezi jua leo upo kesho haupo na wala haina faida yoyote kuwa na tofauti (bifu) wakati wao ni vijana na wanaweza kufanya kazi nyingi za pamoja hasa kibisahara.
"Tuliamua kumaliza tofauti zetu baada ya kugundua tulichokuwa tunakifanya ulikuwa ni utoto, japokuwa mimi sikuwahi kumchukia Diamond Platnumz ila nilikuwa nasubiri wakati wa Mungu ufike tuwe kama zamani na wakati wenyewe ndio huu.
"Ilikuwa ni lazima tumalize tofauti zetu kwasababu asilimia kubwa ya marafiki wa Diamond ni marafiki zangu na marafiki zangu wengi ni marafiki wa Diamond, hakuna aliyetupatanisha ila tulijikuta tu tunazungumza na baadae tukawa sawa.
"Diamond amenipa kazi ya kupanda kwenye majukwaa ya Wasafi Festival hii ni ishara nzuri kwetu baada ya kutokuwa sawa kwa miaka saba," amesema Ommy Dimpoz.