Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dimpoz amlipua baba yake "Sina mapenzi naye"

DIMPOZ NA BABA'KE Dimpoz amlipua baba yake "Sina mapenzi naye"

Wed, 14 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkali wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Dimpoz’ alisema baba yake mzazi alimtelekeza na hakuwahi kumuonesha mapenzi tangu anazaliwa mpaka sasa.

Akizungumza kupitia kipande cha video alichokiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, Dimpoz alisema anaitumia siku yake ya kuzaliwa, kutoa ujumbe kwa wazazi watarajiwa.

“Wazazi tutanakiwa kuwaonesha mapenzi watoto wetu hata kama hatuna kitu. Mimi baba yangu hakunionesha mapenzi kabisa, alinitelekeza lakini sasa hivi anaibuka hataki kusikia lolote anataka ajulikane kama ndiye baba Dimpoz.

“Huu ni ujumbe kwetu mimi nilikuwa mtoto wa nje ya ndoa nilifahamu kabisa kwamba siwezi kurithi hivyo nilijipanga kivyangu na hata haya mafanikio nitakula na wale niliohangaika nao, sina tatizo naye lakini sina mapenzi naye,” alisema Dimpoz.

Baba Dimpoz alifanya mahojiano jana na Clouds TV ambapo alijitambulisha kama baba wa Dimpoz akieleza maisha yake kuwa ni ya hali ya kawaida akiwa anaendesha Bajaj kitendo ambacho Dimpoz amesema ni kumtumia mzee huyo kama kiki ya Fiesta na inamharibia yeye kwa namna moja au nyingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live