Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dimpoz: Nilikunywa sumu

Ommy Dimpoz Ommy Dimpoz

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa Bongo Fleva, Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' amefunguka alivyougua koo miaka michache iliyopita hali iliyosababisha kufanyiwa upasuaji mara mbili huku akiunusurika kupoteza maisha yake kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo wakati huo.

"Kama mnavyokumbuka nilipata changamoto ya kiafya. Sikuwa na Kansa bali nilikuwa nashindwa Kula chakula. Kilikuwa hakishuki.

"Nilifuatilia vipimo hapa nyumbani lakini tatizo halikupatiwa ufumbuzi. Ilihitaji vipimo vya ziada. lIlihitajika kwenda nje ya nchi. Vipimo vikasema kwamba nilikula sumu.

"Hiyo hali ilinisumbua Sana. Nilikuwa najiuliza nilikula wapi sumu? Niliamua ni-focus kwenye matibabu. Changamoto ilikuwa inakuja wakati wa upasuaji ilikuwa ni kupoteza sauti"

"Hiyo hali ilinifanya niwe kimya kufanya Muziki na pia Sitaki presha ya muziki. Labda pengine industry inataka tuvae suruali chini ya makalio. hapana! Siwezi kuwa hivyo," amesema @ommydimpoz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live