Msanii wa Bongo Fleva, Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' amefunguka kuhusu kumaliza tofauti zake na msanii mwenzake Diamond Platnumz ambapo amesema kwamba ilikuwa ni utoto na kwasasa haina maana tena kuendelea kuwa na utofauti.
Dimpoz amesema maisha ya sasa huwezi jua leo upo kesho haupo na wala haina faida yoyote kuwa na tofauti (bifu) wakati wao ni vijana na wanaweza kufanya kazi nyingi za pamoja hasa kibisahara.
“Wakati mwingine ni utoto na ujana mnaweza kujikuta kwenye vutu ambavyo havina kichwa wala miguu, sasa hivi tumeshakua na tunaangalia zaidi maisha na hujui leo upo na kesho hautakuwepo. Hakuna haja ya kuishi kwa kuwekeana vinyongo.
“Ukikaa ukaangalia hakuna sababu kubwa ya msingi kuwafanya muwe katika ugomvi. Tulikutana sisi wenyewe tukazungumza na kuyamaliza kiume. Mimi na Diamond tuna historia huko nyuma kabla ya vitu vingine kutokea, hakuna faida yoyote kuendelea kuwa na bifu.
“Mimi ninaamini sisi ni kama mfano kwa watu wengine, mimi siishi kwenye mambo ya utimu… hata kabla ya utimu mimi nilikuwa naongea nao wote wawili (Diamond na Kiba) vizuri tu, mimi ninamsapoti kila mtu wala sina timu. Ninafocus kwenye biashara zaidi na ninahitaji kufanya kazi na mtu yeyote,” amesema Dimpoz.