OMARY Nyembo au Ommy Dimpoz; ni mkali mwingine wa Bongo Fleva sema tu hachii ngoma mara kwa mara ambaye anasema kuwa, wasichana wengi wanatamani kuolewa na yeye na kila mara amekuwa akipokea maombi yao.
Dimpoz anasema hiyo ni moja ya sababu za kutomuweka wazi mpenzi wake kwani anajua kufanya hivyo atawaumiza wengi.
“Kuna wasichana wengi sana kila siku wanalia nioe mimi, hizo nishazoea, ni kawaida, nina uhakika na watu wengine inawatokea, lakini mimi naweza kuwa baba yao kwenye suala hilo,” anasema Dimpoz.
“Lakini katika suala hilo (kuoa) mimi Muislam naruhusiwa kuoa wanne, kwa hiyo inawezekana hata sasa hivi nina hao wanne wa kuwapima, kwa hiyo time itakapofika haina shida,” anasema, kwa sasa Dimpoz anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa Umeniweza.
Amesema kuwa, kwa sasa hana mtoto, lakini kabla ya mwaka huu kuisha mambo yanaweza kuwa mazuri, yaani kupata mtoto.