Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dimpoz: Bifu la Kiba na Diamond ni pesa, liendelee tu!

DIAMOND ALIKIBA HARMONIZE.jpeg Diamond Platnumz na Dimpoz.

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa Bongo Fleva, Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amesema bifu la masupastaa wa muziki nchini, Diamond Platnumz na hasimu wake, Alikiba liendelee tu lakini liwe kwa ajili ya kutengeneza pesa zaidi kuliko kurumbana.

Dimpoz ambaye ni swahiba wa Diamond na Alikiba amesema hayo wakati akihojiwa na The Switch ya Wasafi Fm ikiwa ni siku chache baada ya kutangaza kupatana na rafiki yake Diamond.

“Kinachotakiwa makampuni yaweke pesa ipigwe ‘Nani Mkali’ watu waingize pesa na ubishi uishe. Tuangalie huyu anapiga vocal huyu anaruka sarakasi tutengeneze pesa, kila mmoja ana watu nyuma yake sijui nini kinashindikana.

“Mimi ukiniuliza sasa hivi bifu life au lisife nitakujibu lisife lakini lizalishe pesa. Na hili tamasha la ‘Nani Mkali’ liende mikoa yote. Kama kutukanana na kutoleana mapovu imekaa miaka na miaka lakini hakuna fainda, twende stejini nani mkali apige ngoma zake.

“Hii haihitaji hata watu wa kufungua shoo, MC anafungua shoo anapanda mtu wa kwanza anapiga ngoma zake nne, akimaliza anapanda wa pili anapiga nne, hivyo hivyo wana mpaka ngoma hata 20 kisha tunawauliza mashabiki wanachagua mkali, baadaye linapigwa dude kubwa Dar, asipopatikana tunarudi tena mwakani.

“Hapo wadhamini watapata faina, wanahabari watapata contents, wadhamini mimi nitazungumza nao na wao kama wasanii nitawaambia wapige kazi. Kiba nitamwambia bro yule mtoto hakuna kumchekea na Diamond nitamwambia zile piano zako zilie mpaka Kiba asikutoe kwenye reli.

“Diamond na Alikiba ni kama Simba na Yanga lakini kwa nini timu hizi kila siku zinakutana na zinafanya kazi zinaingiza pesa?,” amesema Dimpoz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live