MSANII wa kizazi kipya, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amesema kwa sasa tasnia ya ubunifu wa mavazi nchini inafanya vizuri tofauti na zamani.
Alisema miaka ya nyuma watu wengi waliokuwa wanafanya biashara hiyo walikuwa hawaipi thamani kubwa kama wanavyofanya sasa.
Ommy Dimpoz alisema: “Kiukweli imekuwa na kwa muda mrefu nimekuwa nikifanya kazi kwa ukaribu na watu wengi wanaofanya shughuli za ubunifu wa mavazi.”
“Nafanya kazi na watu ambao wanafanya mambo ya fasheni wanajielewa na wamekuwa wakizingatia utanzania na kuendelea kuboreka kila iitwapo leo,” alisema.
Ommy Dimpoz amewaomba wazazi kuwaacha huru watoto wao kushiriki sanaa hiyo akisema wana nafasi kubwa ya kurithi na kuendeleza utamaduni wa Mtanzania kwa kuvaa mavazi yenye asili ya nchi yao.
Alisema hata kwenye shughuli zao za muziki wasanii wana wajibu wa kuvaa mavazi yenye ubunifu tofauti kwa sababu mashabiki wanafurahia.