Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dimond afanya kufuru nyingine, anunua helkopta

MONDI KOPTA Dimond afanya kufuru nyingine, anunua helkopta

Thu, 11 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameweka bayana kuwa kwa sasa, amenunua helkopta yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram (Insta-Story) jana Agosti 10, 2022, Diamond ndio alitupia ujumbe mfupi sana akimshukuru Mungu kwa kumwezesha kununua helkopta.

"Mungu ni mwema, nimenunua helikopta leo."

Ikumbukwe, hivi karibuni Diamond alithibitisha kuwa tayari amenunua ndege binafsi (private jet) hivyo huu ni muendelezo wa kufuru anazozifanya Diamond. Mbali na hayo, Diamond pia ni msanii anayeongoza Bongo kwa kumiliki mandinga ya bei mbaya ikiwemo Rolls Royce.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live