Mfanyabiashara na tajiri wa Marekani Diddy alirejea studio baada ya zaidi ya muongo mmoja kwa albamu ya tano ya studio.
“Niliondoka kwa muda kidogo, nikapitia mambo mengi maishani, kisha nikapata wito huo siku moja kutoka kwa Mungu. Alikuwa kama, ‘Wakati umefika,’” Mshindi huyo mara tatu wa Grammy alisema sauti nyororo aliyosikia papo hapo ilimchochea kuelekeza fikira zake tena kwenye kutengeneza muziki wake mwenyewe tena.
Siku ya Ijumaa (Sep. 15), Diddy ataachia albamu yake mpya iitwayo “The Love Album – Off the Grid.” project yake ya tano ya studio unajumuisha karibu wasanii 30 wakiwemo Mary J. Blige, Justin Bieber, The Weeknd, H.E.R., Babyface, John Legend, Busta Rhymes, Summer Walker, Teyana Taylor, Coco Jones na Jazmine Sullivan.
hii ni project yake ya kwanza ya studio ya pekee tangu mwaka wa 2006, “Press Play,” ambayo ilikuwa na nyimbo 10 bora zaidi ikiwa ni pamoja na “Last Night” na Keyshia Cole na “Come to Me” akimshirikisha Nicole Scherzinger.
“Nilikuwa kama, ‘Nataka kutengeneza R&B.’ Nilikuwa nikijiuliza swali: ‘Ikiwa ungelazimika kufanya jambo moja kwa maisha yako yote, ungefanya nini?’ Na hiyo ingekuwa kufanya muziki.
Ni nini kingekuletea furaha? Huo ungekuwa muziki. Ni nini kimekusaidia kuwa na matokeo mazuri juu ya ulimwengu? Huo ungekuwa muziki.’ Lakini sikuwa nikifanya muziki. Kuanzia sekunde hiyo na kuendelea, niliruka moja kwa moja kwenye mradi huu, ambao ni kurudi kwenye upendo wako.