Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diddy avunja ukimya tuhuma za ubakaji zinazomwandama

Diddy Akabiliwa Na Msala Mwingine Diddy avunja ukimya tuhuma za ubakaji zinazomwandama

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki P Diddy amevunja ukimya wa taarifa zinazoendelea dhidi yake kuhusu madai ya wanawake wanaojitokeza kufungua kesi za kuwanyanyasa kingono, udhalilishaji na ubakaji miaka ya nyuma.

Diddy anasema taarifa hizo zinalengo za kutaka kuua sifa zake, kumchafua na kumuharibia Legacy yake aliyoitengeneza.

“Kwa wiki kadhaa zilizopita nimekaa kimya kuangalia watu wakijaribu kuharibu sifa zangu na legacy yangu, Madai ya taarifa hizo kwa watu binafsi dhidi yangu wamekuwa wanataka malipo.

“Acha niweke wazi kabisa, sikufanya mambo yoyote ya kutisha yanayodaiwa. Nitapambana kwa ajili ya jina langu, familia yangu na kwa ukweli” ujumbe wa Diddy kuhusu taarifa hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live