Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diddy ashindwa kuhudhuria mahafari ya binti yake

Maafisa Wa Usalama Wapekua Nyumba Za Sean 'Diddy' Combs Diddy ashindwa kuhudhuria mahafari ya binti yake

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkali wa Hip-hop kutoka Marekani Diddy ameripotiwa kuwa hatokuwepo kwenye mahafari ya binti yake aitwaye Chance (17) huku wadau wakieleza kuwa hatohudhuria katika sherehe hiyo kufuatia na kesi zinazomkabili.

Kwa mujibu wa Tmz mahafali ya #ChanceCombs yatakayofanyika katika Shule ya Sierra Canyon huko Los Angeles yatahudhuriwa na familia ya Kim Porter pamoja na mama mzazi wa Chance, Sarah Chapman.

Hii inakuwa mara ya pili kwa #Diddy kutohudhuria kwenye matukio makubwa ya watoto wake kwani wiki iliyopita alishindwa kuhudhuria kwenye shughuli ya tangazo la biashara ya watoto wake mapacha #Jessie na D'Lila.

#Diddy amekuwa akiandamwa na kesi za unyanyasaji wa ngono toka mwishoni mwa mwaka jana, ambapo mpaka kufikia sasa wanasheria wake wanaendelea kupambana na kesi hizo mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live