Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diddy akabiliwa na msala mwingine

Diddy Akabiliwa Na Msala Mwingine Diddy akabiliwa na msala mwingine

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Msanii wa muziki wa rapper Sean "Diddy" Combs maarufu kama P Diddy ameshtakiwa na mwanamke ambaye anasema alimwekea dawa za kulevya na kumdhalilisha kingono mwaka 1991.

Katika kesi iliyoonekana na BBC, mlalamikaji anasema unyanyasaji huo ulifanyika wakati alipokuwa ameenda kukutana na rapper huyo.

Kesi nyingine ya unyanyasaji wa kingono iliyokuwa inamkabili iliyowasilishwa na mwimbaji wa R&B na mshirika wake wa zamani Casandra "Cassie" Ventura ilimalizika hivi majuzi.

Mwakilishi huyo wa rapper alitaja madai ya hivi punde kuwa "yakubuniwa na sio ya kweli".

"Huu ni unyakuzi wa pesa tu na si chochote zaidi," msemaji wake alisema katika taarifa kwa BBC siku ya Alhamisi.

Katika kesi hiyo, mlalamikaji, Joi Dickerson-Neal, anasema kwamba alimfahamu Bw Combs - ambaye pia anajulikana kwa jina la kisanii Puff Daddy au P Diddy - kupitia kwa marafiki. Pia alikuwa ameonekana katika moja ya video zake za muziki.

Kulingana na malalamiko hayo, mnamo tarehe 3 Januari 1991, "bila kusita" alikubali kukutana na Bw Combs kwenye mkahawa wa Harlem ambapo "alimlazimisha" ili kuwa naye alipokuwa akishughulikia mambo yake mengine kidogo jijini".

Anasema kwamba wakati huo alitiliwa dawa na rapa huyo "iliyosababisha kuwa katika hali asiyoweza kujifanyia maamuzi ambapo hakuweza kujitegemea au kutembea".

Baadaye alimpeleka hadi mahali alipokuwa akiishi, ambapo alimnyanyasa kingono, kwa mujibu wa kesi hiyo.

Anasema baadaye aligundua kuwa alirekodi tukio hilo kwa siri na kuwaonyesha watu wengine kadhaa.

Kesi hiyo inaelezea jinsi baada ya unyanyasaji huo, maisha yake yaliingia "doa" na kuharibika - alitatizika na afya yake ya akili na hivi karibuni aliacha chuo kikuu.

Hatua hiyo ya kisheria inawadia saa chache kabla ya Sheria ya Watu Wazima Walionusurika ya New York - ambayo inaruhusu waathiriwa wa uhalifu wa ngono kushtaki baada ya sheria iliyokuwa ikizuia hatua hiyo - kumalizika tarehe 24 Novemba.

"Mteja wetu hajaweza kuepuka athari zinazoendelea za madhara yaliyosababishwa na Combs miaka mingi iliyopita," alisema Jonathan Goldhirsch, mmoja wa mawakili, katika taarifa.

"Kupitia Sheria ya Watu Wazima Walionusurika, anaweza kufika mahakama na hatimaye kutafuta haki yake."

Hii ni kesi ya pili ya unyanyasaji wa kijinsia kuletwa dhidi ya Bw Combs mwezi huu.

Bi Ventura alimshutumu gwiji huyo wa muziki kwa ubakaji na ulanguzi wa ngono katika kesi iliyowasilishwa wiki jana. Alidai kuwa mwanamuziki huyo alimbaka na kumpiga kwa zaidi ya miaka 10 kuanzia akiwa na umri wa miaka 19 na yeye akiwa na miaka 37.

Wawili hao waliafikiana kutatua kesi hiyo siku moja baada ya kuwasilishwa.

Hata hivyo, Bw Combs amekanusha madai ya Bi Ventura na wakili wake alisema uamuzi wa kusuluhisha hilo haukuwa kukubali makosa.

Chanzo: Bbc