Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diddy ajibu tuhuma za Will Smith na Jada kutaka ‘Threesome’ na Lopez

Will Smith Na Jada Diddy ajibu tuhuma za Will Smith na Jada kutaka ‘Threesome’ na Lopez

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diddy alishea jibu lake kufuatia madai ya mlinzi wake wa zamani kwamba ilibaki kidogo apigane na Will Smith kuhusu Jennifer Lopez.

Jumatatu (Oktoba 30), mogul huyo wa Bad Boy alionekana kwenye show ya Jimmy Kimmel Live! ili kujadili kuhusu albamu yake mpya, The Love Album: Off The Grid.

Wakati wa mazungumzo, mtangazaji aliibua madai ya Gene Deal kwamba Will na Jada Pinkett-Smith walikuwa na matumaini ya kumvuta J.Lo ili kufanya nae mpenzi ya watu watatu (wanawake wawili na mwanaume mmoja ).

Baada ya kumkodolea macho Kimmel kwa maneno ya ukali akijibu swali hilo la kijasiri, mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 53 alivunja ukimya na kusema: “Lo, show hili imekuwa na kichaa tangu mara ya mwisho nilipokuwa hapa … umesikia hivyo kweli? sijui unaongea nini. Jimmy, nilifikiri sisi ni marafiki.”

Stori hiyo iliibuliwa hivi majuzi na Deal (aliyekuwa mlinzi wa Diddy) wakati wa mahojiano na The Art of Dialogue mwezi uliopita, ambapo alikumbuka hisia kali za Puff baada ya kuhisi kuwa staa wa Men In Black na mkewe walikuwa wakijaribu kumtongoza mpenzi wake.

Haijulikani ni lini hasa mgongano huo unaodaiwa ulitokea, lakini Diddy na Jennifer Lopez walikuwa na mahusiano kati ya mwishoni mwa 1999 na mapema 2001 baada ya kukutana kwenye utengenezwaji waa video ya muziki; kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa tukio hilo lilitokea ndani ya muda huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live