Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dida amchamba Wolper "ulizoea kuhongwa, mimi sidangi"

Uwoya Dida' Dida amchamba Wolper

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mdau wa masuala ya burudani na mtangazaji wa Wasafi FM, Dida Shaibu amemtupia dongo msanii wa Bongo Movies, Jackline Wolper akidai kuwa kwa sasa mwanadada huyo ameishiwa pesa na anaishi maisha magumu.

Dida amefunguka hayo baada ya wawili hao kupishana na kuanza kuchambana kupitia mitandao ya kijamii.

"Sawa nimekubali nyumba yangu ninayoishi ni sawa na banda la wafanyakazi wa Wolper, sawa lakini je! Ushawahi kuiona nyumba ya Wolper? Labda nimwambie tu Wolper kwamba mimi ni mwanamke na ni mwanamke haswaa niliyekamilika, nimeweza kujenga kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, umenielewa?

"Hizo gari zangu unazoona hazifai mimi nimenunua kwa jasho langu sijadanga, naomba utambue kwamba mimi sio mdangaji, sijadanga nimenunua kwa pesa yangu, kwa jasho langu na nyumba yangu nimejenga kwa kazi yangu.

"Sasa basi, ujue kabisa mimi ni mwanamke mpambanaji na mtafutaji haujawahi kunikuta hata siku moja mimi nadanga, mimi najivunia kwa sababu nimepambana mwenyewe sina mapedeshee.

"Wolper una stress nakujua hali yako ya kimaisha kwa sasa sio nzuri, hata huko kuuza sabuni na mafuta sio kupenda kwako ni ugumu wa maisha umekufanya upande juu ya meza kama mnenguaji.

"Kwa kinywa chako mwenyewe umekubali kwamba umehongwa sana mamilioni na mapedeshee ukazichezea pesa umekuja kushtuka ukubwani, umri ushaenda huwezi tena kupata pedeshee wa kukupa mamilioni ndio maana una stress, maisha magumu huelewi.

"Mimi nimekuzidi mbali mdogo wangu, nimekuzidi mbali mnoo, ni kwa vile tu ukishazoea kuhongwa huwezi kuthamini kitu cha mwanamke mwenzako mpambanaji unamuonea wivu.

"Juzi tu hapa nimekupa mchongo wa mamilioni na nikakwambia usinipe hata mia hiyo pesa unayotaka kunipa wanunulie wanao chakula wapishane chooni maana tunajua uko mwenyewe

"Nimeshangaa kuona unanisema tena kwa mkazo, mimi sio levo zako, nimekuzidi mbali mnoo, tafuta pesa angalau utoke kwenye hiyo hali uliyonayo sasa," amesema Dida Shaibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live