Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dida: Nina maombi mengi ya ndoa

Didaaa Dida: Nina maombi mengi ya ndoa

Sat, 10 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa Wasafi, Dida Shaibu amesema baada ya kuachana na aliyekuwa mumewe Meya Omari Kumbilamoto, amepokea maombi mengi ya wanaume wanaoonesha nia ya kutaka kumuoa.

Dida amefunguka hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi TV ambapo alieleza sababu ya kuachana na mumewe huyo ilikuwa ni kupishana tabia.

“Alinionesha makucha yake baada ya kuingia kwenye ndoa so ikabidi tuachane na sasa nipo singo, nainjoi maisha,” alisema Dida na kuongeza:

“Nimepokea maombi mengi tu ya ndoa watu wananipenda sana sababu mimi ni mtu mzuri mwanamke mtafutaji.”

Dida hakueleza kama kwenye hayo maombi yupo mmoja wao ambaye anaweza kumpa nafasi au la zaidi ya kusema amepokea maombi mengi ya kuolewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live