Mtangazaji Dida Shaibu ‘Dida’ amesema mfalme wa Taarabu Bongo, Mzee Yusuf kamwe hawezi kumuoa kama ambavyo amekaririwa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari.
Akizungumza na Wasafi TV, Dida amesema, amepokea maombi mengi ya ndoa lakini hawezi kuolewa mke wa pili hata iweje kwani yameshamkuta huko nyuma alipoolewa na Meya Omari Kumbilamoto.
“Siwezi kamwe kuolewa mke wa pili. Waolewe tu hao wanaotaka kuolewa mke wa pili mimi hapana,” alisema Dida.
Dida alimaliza kwa kusema amesikia Mzee Yusuf akisema amewahi kuwa na mahusiano naye na kwamba anataka kumuoa jambo ambalo si la kweli na haiwezekani.
“Yule anatafuta tu kiki za mjini si unajua tena mtu ukitaka kutoka mjini lazima uzungumzie watu kama sisi. Mzee Yusuf ni mtu ambaye tunafahamiana, tunaheshimiana na namheshimu mke wake lakini hawezi kunioa mimi na hatujawahi hata kuwa na mahusiano,” alisema Dida.