Kama haupo connected na mbanga za Uswahilini, ungemwona anapayuka redioni. Ungeulizia namba, ungestaajabu. Khadija Shaibu "Dida", the queen of uswazini.
Dida, aliligundua mapema gape lililokuwepo baina ya mainstream na wanawake wa Uswahilini. Alilifanyia kazi. Akaziba gape. Fedha zikamfuata alipo. Akawa Malkia wa Uswahilini.
Misele ya Mtaa kwa mtaa, kurusha matangazo live kutoka kitongoji hadi kitongoji, hakuna aliyethubutu kusogelea anga za Dida. Alikuwa wa moto sana. Aliishika mitaa kuliko yeyote kabla na baada.
Times FM katika prime yake, Mitikisiko ya Pwani ya Dida, namba moja, probably Dida akawa ndiye mtangazaji wa kike anayelipwa fedha nyingi kuliko yeyote Tanzania. Biashara zilimfuata. Kampuni za kibiashara hadi taasisi za umma, zilipigana vikumbo kutangaza kupitia Dida na Mitikisiko ya Pwani.
Dida, aliujengea thamani kubwa muziki wa Taarab redioni, kisha concerts hadi festivals za Mitikisiko ya Pwani. Michambo na mipasho, ni nakshi za Taarab kiutamaduni. Dida, akawa mwanamke bingwa wa kuchamba na kupasha. Alikuwa sauti ya akina mwajei, kurusha mivuguvugu ya rohoni kwa mahasimu wao interio-to-interior.
Huwezi kuishika mitaa na kujua namna ya kusafiri na wanawake wa Uswahilini kwa ukubwa, tena kwa miaka, mithili ya Dida alivyoweza, bila kipaji, elimu na maarifa makubwa. Dida, alikuwa na kipaji kikubwa, maarifa mengi, halafu mwanazuoni wa kitaa.
Bila shaka, Wasafi Media, waliona Dida ni lift nzuri ya kukwea viwango vya kuishika mitaa, ndiyo sababu walimpandia bei, wakamchomoa Times FM, wakambeba.
Hatima ya binadamu duniani ni siri ambayo Mungu ameificha mbali. Miongo miwili iliyopita, nani alijua mwisho wa career ya Dida, ungekuwa kifo, na mauti yangemkuta akiwa Wasafi? Mungu anaujua mwisho, binadamu ni kipofu.
Dida, mcheshi sana, rafiki wa yeyote. Kupitia kipawa na nafasi yake, aliweza kutambulisha na kung'arisha vipaji vingi katika utangazaji. Pengine, wito wake duniani ulikuwa huo na akautimiza.
Duniani, kila mja ni mpangaji asiyelipa kodi, hivyo hakuna mkataba wa uhai. Wakati wowote, mwenye dunia yake akiamua, anakuchukua, unaipisha sayari. Ndivyo imekuwa kwa Dida. Itakuwa hivyohivyo kwangu.
Ndimi Luqman MALOTO