Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diana Armstrong ndiye binadamu mwenye kucha ndefu zaidi Duniani

Diana Armstrong  (5).jpeg Diana Armstrong ndiye binadamu mwenye kucha ndefu zaidi Duniani

Wed, 1 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diana Armstrong mkazi wa Minnesota, nchini Marekani anashikilia rekodi ya kuwa binadamu mwenye kucha ndefu zaidi duniani ambapo ana kucha zenye urefu wa sentimita 1,306.58 sawa na futi 42.

Rekodi hiyo iliyothibitishwa na The Guiness Book of Records, imeeleza kuwa Diana hajakata kucha tangu 1997 na hana mpango wa kukata tena kucha zake, ambapo alieleza kuwa alifanya hivyo, kwa ajili kumuenzi binti yake ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 16.

Diana alieleza kuwa yeye na binti yake walikuwa wakishirikiana kutengeneza kucha zao kwa pamoja.

Awali rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Lee Redmond (Marekani) tangu 2008, ambaye alikuza kucha zake ambazo zilifikia urefu wa sentimeta 865 sawa na futi 28.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live