Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond na mkasa wa TX Moshi

DIAMOND Diamond na mkasa wa TX Moshi

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

KABLA ya muziki wa Bongofleva kuliteka soko la muziki hapa nchini, dansi ndiyo ulikuwa muziki namba moja.

Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) iliutumia muziki wa dansi kama ambavyo redio za sasa zinavyoutumia muziki wa Bongofleva.

Ukiacha taarifa ya habari, matangazo ya vifo, michezo na vipindi vya taarifa kama Majira vipindi vilivyobaki vyote vilipiga muziki wa dansi kuanzia Kombora saa 11:30 alfajiri hadi Usiku wa Raha saa 5 usiku.

Wakati huo RTD ilikuwa haikeshi, matangazo yalifunguliwa saa 11 alfajiri na kufungwa saa 6 usiku kila siku. Sasa katika vipindi vyote ilikuwa haiwezekani ukakosa kusikia sauti ya fundi mmoja aliyeitwa TX Moshi William. Mwamba huyu bingwa wa uimbaji na utunzi alipitia bendi kadhaa kama Safari Trippers, Polisi Jazz, UDA Jazz, Vijana Jazz na mwisho akakita nanga Juwata Jazz.

Alijiunga na Juwata Jazz Band (ambayo baadaye ikawa Ottu) mwaka 1982 na kuungana na nyota wengine kama Nico Zengekala, Mkenya aliyetokea Les Quban (bendi ya Juma Kilaza).

Ujio wake ndani ya Juwata Jazz ukamfanya mtangazaji maarufu wa vipindi vya burudani wakati huo, Julius Nyaisanga ‘Uncle J’ (marehemu) kumfananisha na watalaamu wa kimataifa waliokuja Tanzania miaka hiyo.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz