Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond na Zuchu wavuka mipaka ya aibu

Diamond Zuchu K Diamond na Zuchu

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diamond Platnumz na Zuchu; ni mastaa wakubwa wa muziki nchini Tanzania ambao penzi lao sasa limevuka mipaka.

Yapo maswali yanayoulizwa na baadhi ya mashabiki wao hasa baada ya kusambaa kwa video ya Zuchu akishangiliwa na vijana wa bodaboda wakimuita semeji kwa kuwa siyo siri kwamba mapenzi yake na Diamond hayafichiki tena.

Wapo wanaohoji kuwa, ni lini watu wataamini kwamba Diamond na Zuchu ni wapenzi au mpaka wapeane mimba?

Kila dalili zinaonesha kwamba Diamond na Zuchu wapo penzini, hii siyo biashara tena wala kutafuta kiki, lakini vyanzo vya ndani vinathibitisha kuna jambo zito linaendelea kati yao.

Miongoni mwa video zao zinazotrendi kwa sasa ni ile ambayo inaonesha Zuchu akilishwa jojo au pipi mdomoni na Diamond mbele ya Chawa Baba Levo. Kwenye video hiyo, usipoangalia vizuri video hiyo, utadhani wanadendeka ila ukweli ni kwamba wanalishana pipi kwa midomo yao.

Wenye makasiriko wanasema kuwa, huko ndiko kuvuka mipaka kwani haiwezekani ukamlisha mtu kupitia mdomo kisha ukakana kwamba hutoki naye kimapenzi.

Wanasema kuwa, mbaya zaidi mpaka sasa haijulikana mpenzi wa Diamond mbali na Zuchu kama ambavyo haijulikani mpenzi wa Zuchu mbali na Diamond.

Wapo wanaosema kuwa, wataamini kwamba Zuchu hatoki na Diamond baada ya kumjua mpenzi wa Diamond na mwanaume wa Zuchu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live