Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond na Rayvanny watajwa Forbes

Diamond Rayvanny Nm Diamond na Rayvanny watajwa Forbes

Wed, 24 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jarida maarufu la @forbesafrica limeorodhesha idadi ya Celebrities 20 Barani Afrika wenye ushawishi na mchango mkubwa kwenye tasnia ya muziki wa Afrika.

Jarida hilo limeangazia namna ambayo muziki wa Afrika unakuwa hususani kupitia mafanikio ya wasanii mbalimbali barani humo.

Mambo yaliyotazamwa na kujitanua kibiashara na kuvuka mipaka ya Bara la Afrika na kufanya makubwa nje ya Bara hilo, utajiri wao kwenye digital platforms na mitandao ya kijamii, bila kusahau tuzo kubwa na mambo mengine ya kimuziki.

Kwa upande wa Tanzania ni wasanii wawili tu ndiyo wameingia kwenye orodha hiyo, Rayvanny ambaye Mama Tetema aliyofanya Maluma imekaa hadi kwenye Billboard Charts pamoja na kuwa Gold Certified nchini Marekani na utajiri mkubwa kwenye digital platforms zake ambapo rayvanny anatajwa kuwa ndio msanii anayeuza zaidi kazi zake kupitia digital platforms kuliko msanii yoyote nchini Tanzania.

Kwa upande wa Diamond Platnumz kwa mujibu wa BET, ana dozen za tuzo na nominations nyingi kubwa ikiwemo Best International Act. Mondi ni msanii mwenye tuzo nyingi Afrika Mashariki na wa 5 chini ya jangwa la Sahara.

Mwaka 2020, Shirika la Habari la BBC waliripoti kuwa ndiye msanii wa kwanza chini ya jangwa la Sahara kufikisha views Bilioni 1 katika mtandao wa YouTube, akitajwa kama msanii aliyefanikiwa kufanya kazi na makampuni makubwa yaliyopo duniani kote kama Coca Cola na Pepsi.

Wasanii wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni pamoja na Angelique Kidjo, Burna Boy, Nasty C, Tiwa Savage, Davido, Wizkid, 2Face/2Baba Idibia, Fally Ipupa, Yvonne Chaka Chaka, Major League Djs, Master Kg na wengine.







Chanzo: www.tanzaniaweb.live