Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond na Mr Blue kuachia ngoma leo

Diamondplatnumz 1706191920008.jpeg Diamond na Mr Blue kuachia ngoma leo

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki wa hip-hop Mr Blue na nyota wa muziki #Diamondplatnumz wanatarajia kuachia jiwe jipya leo Januari 25.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mondi ameweka wazi ujio wa jambo jipya kwa ku-post picha akiwa na Blue, na kuisindikiza kwa ujumbe usomekao, "Simba ft Nyani Zee, saa sita kamili usiki leo".

#MrBlue amekuwa kimya bila ya kuachia ngoma kwa miezi saba sasa, ngoma yake ya mwisho ilienda kwa jina la 'Amerudi' alimshirikisha Jux na hadi sasa inawatazamaji 91k kwenye mtandao wa YouTube. Kwa upande wa #Mondi ngoma yake ya mwisho alitoa miezi miwili iliyopita iliitwa Pounds & Dollars, alimshirikisha Wouter Kellerman. Mjini YouTube inawatazamaji 1.7 milioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live