Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond na Harmonize wanavyochuana kapo bora Bongo!

DIAMOND VS HARMONIZE Diamond na Harmonize wanavyochuana kapo bora Bongo!

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hakika kwa sasa, unapozungumzia kapo bora ya mastaa harakaharaka itakujia kapo ya Harmonize na Kajala. Ni kapo ambayo iliibuka, ikapotea na sasa imerudi kwa kasi hatari.

Lakini ukiachana na hiyo, kapo nyingine inayokuja kwa kasi ni Diamond na Zuchu. Wawili hao licha ya kuwa hawajatusanua mazima kwamba wanaangusha rumu moja lakini viashiria vyote kwa sasa vinaonesha kwamba wana zaidi ya urafiki wa mtu na bosi wake.

Video imevuja jana ikimuonesha Diamond akiwa zake Ufaransa, big boss huyo wa Wasafi akimfanyia shopping mwandani wake huyo ambaye pia ni memba wa Wasafi.

Sasa gumzo kwa sasa, ni kapo ipi bora kati ya hizi mbili? Harmonize tunaona balaa lake, amemzawadia ndiga Kajala ambayo ina plate number ya jina lake na kama hiyo haitoshi, wiki yake ya bethidei amemfanyia kufuru si ya kitoto.

Amemtoa out ya nguvu mbugani, amemlisha vizuri na kumuonesha kwamba kweli anastahili bethidei yenye hadhi ya kistaa.

Tunamfahamu Diamond naye huwa sio kinyonge linapokuja suala la mahusiano, wacha tumpe muda arejee nchini na watakapoamua rasmi kuonesha ‘mahaba’ yao tunajua dunia itasimama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live