Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond kuwafuta wafanyakazi wa Wasafi na mlinzi wake kisa umeme

Diamondplatnumz 1690377883709.jpeg Diamond Platnumz.

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa Wasafi FM na chawa nambari moja wa msanii Diamond Platnumz, Baba Levo amemshauri msanii huyo kuwafuta kazi wafanyikazi wa Wasafi pamoja na mlinzi wake wa kibinafasi baada ya shoo yao ya mkoa wa Mtwara kukumbwa na hitilafu hadi umeme kupotea.

Baba Levo kupitia Instagram yake alisema kwamba kilichotokea katika shoo hiyo ya wikendi kusababisha Diamond kushindwa kutumbuiza ni tatizo la jenereta lililosababishwa na umeme na ambalo lingezuilika mapema.

Baba Levo alisema kwamba Diamond alikwenda hasara kubwa sana kwa kutowatumbuizia watu wa Mtwara mpaka kuridhika, akiahidi kwamba tayari yeye binafsi kama chawa ameanzisha uchunguzi kujua kama tatizo lile kulikuwa na mkono wa mtu au kuzembea kazini.

“Tunachunguza tuone ni nani aliyezembea kazini, au kama ni jenereta lenyewe hakuna shida. Lakini mimi nimemshauri Diamond Platnumz awafukuze kazi watu wanne, kama sio watatu, wengine ni vionozi wa Wasafi media, lakini pia amfukuze baunza au mlinzi wake,” Baba Levo alisema.

Alitetea ushauri huo wa kufutwa kwa baunsa wa Diamond akisema kuwa kitendo cha kumruhusu bosi wake kutumbuiza gizani mbele ya umati bila kumlinda ni kosa la uhaini.

“Kwa kitendo cha kumruhusu Diamond kutumbuiza gizani tena mbele ya umati uliojaa bila kujua kama kuna mtu yeyote anaweza kurusha kitu chochote kibaya kikampata msanii na madhara yakawa mabaya.

"Ni mara mia mlinzi angesimama mbele ya ya Diamond, ili aendelee kutumbuiza nyuma. Lakini mlinzi alikaa nyuma akamuacha Diamond kama ndiye kiberenge kule mbele anaimba. Haya ni makosa,” amesema Baba Levo.

Wakati wa kutumbuiza kwenye shoo hiyo katika mwendelezo wa tamasha la Wasafi Festival linaloendelea katika mikoa kadhaa nchini Tanzania, umeme ulikatika na Diamond akalazimika kutumbuiza gizani huku watu wakilalamika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live