Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond kumvisha pete ya uchumba Tanasha?

64331 Pic+tanasha

Tue, 25 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msanii maarufu wa muziki Tanzania, Nasseb Abdul maarufu Diamond amesema atafanya tukio kubwa Julai 7 mwaka 2019 maeneo ya karibu na Mwenge jijini Dar es Salaam.

Diamond ameyasema hayo leo Jumanne Juni 25, 2019 alipokuwa akitangaza uzinduzi wa Tamasha la Wasafi linalotarajia kuanza kutimua vumbi la burudani Julai 12 wilayani Muleba mkoani Kagera.

Staa huyo aliulizwa kuwa lini atafunga ndoa na Tanasha Donna ambaye kwa sasa ni mama kijacho, badala ya kujibu swali hilo alisema kuwa :

“Subirini. Nimewaambia Julai 7, 2019 kutakuwa na tukio kubwa maeneo ya Mwenge Mwenge hapo, meza zitakuwa 10 tu, tano kati ya hizo zitauzwa Sh500,000 kila moja, sasa huwezi kujiuliza hili litakuwa tukio kubwa la namna gani, msiwe na papara subirini siku hiyo mtapata majibu,” amesema Diamond.

Msanii huyo ana watoto watatu, wawili akiwa amewapata na Zarina Hassan raia wa Uganda na mmoja amempata na Hamisa Mobeto, ilihali kuna taarifa kuwa mpenzi wake Tanasha raia wa Kenya ni mjamzito.

Staa huyo pia alitumia hafla hiyo ya uzinduzi kuwatia moyo wachezaji wa Taifa Stars waliopo nchini Misri kwenye michuano ya  Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa kuwataka waendelee kupambana kufa na kupona.

Pia Soma

Amesema wakati wa kuwania kufuzu kushiriki michuano  ya (AFCON), ‘Taifa Stars’ iliifunga timu ya mashemeji zake Uganda, lakini safari hii kwa mara ya kwanza atambadili uraia mpenzi wake huyo (Tanasha) kutoka Kenya kwa kumshawishi ashangilie timu ya Tanzania.

“Atavaa jezi ya Tanzania na ataishangilia Taifa Stars, nitamshawishi, msiwe na hofu wifi yenu atawaunga mkono,” amesema Diamond.

Chanzo: mwananchi.co.tz