Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond kufanya mambo saba akisherekea siku yake ya kuzaliwa

20777 Diamond+pic TanzaniaWeb

Thu, 4 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye Oktoba 2 alisherehekea kutimiza miaka 29, amepanga kufanya mambo saba kwa wiki nzima mengi yakiwa ni shughuli za kijamii.

Diamond anayetamba na wimbo Jibebe ameyataja mambo hayo kuwa kwanza ni kuzungumza na vijana wanaoishi Tandale jijini Dar es Salaam na kuwaeleza njia alizopitia hadi kupata mafanikio aliyo nayo sasa.

Shughuli nyingine atakayoifanya ni kutoa kadi za  bima ya afya kwa watoto 300 katika eneo hilo hilo la Tandale.

Kama vile haitoshi msanii huyo amewakumbuka kina mama 200 ambapo hawa anasema atawapatia mikopo ya biashara.

Msanii huyo baba wa watoto watatu Tiffah, Nillan na Dylan, anabainisha kuwa upande wa elimu hatausahau kwani anatarajia kukarabati shule zote zilizopo Tandale, huku akianza na ile aliyosoma.

Kwa vijana pia hataishia kuzungumza nao tu, kwani atawagawia baadhi yao bodaboda 20 lengo likiwa kuwawezesha kujiajiri.

Katika hili, msanii huyu anayefuatiliwa na  watu zaidi ya milioni tano kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, anasema  kila siku boda hizo zitatakiwa kuzalisha Sh10,000 kila moja na baadaye kuwezesha kununua boda nyingine ambazo zote hizo zitakuwa katika uangalizi maalum.

Kama unavyojua raha ya sikukuu ni kula na kunywa, basi watu wa Tandale katika siku zote hizo hawataishia tu kupewa msaada bali watajumuika na msanii huyu katika kula ambapo anatarajia kuchinja ng’ombe.

Baada ya hapo anasema sherehe hiyo itahamia baharini katika boti ya kifahari na kula bata na marafiki pamoja na wafanyakazi wake wapatao 60.

Chanzo: mwananchi.co.tz