Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond kufanya balaa Ureno

Diamond Platnumz(21).jpeg Diamond Platnumz

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota ya muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ inazidi kung’ara baada ya kutangazwa kuwa mmoja ya wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Afro Nation akiwa ni msanii pekee kutoka Afrika Mashariki.

Tamasha hilo kubwa linalofanyika kila mwaka, litafanyika mwakani kati ya Juni 26 hadi 28 katika mji wa Portimao, Ureno na staa huyo wa ‘Achii’ aliyoimba na Koffi Olomide ametajwa kuwa mmoja wa watakaotumbuiza sambamba na wakali wengine kutoka mataifa mengine.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa tamasha hilo, umewataja wakali watakaoshiriki ni pamoja na Rema, Asake, Tyla, Seyi Vibez, The Compozers, Omah Lay, Flavour, Ninho, J Hus na wengine sambamba na madj maarufu duniani.

Mondi aliyeanza muziki  2006 kabla ya kutambulika rasmi 2009 amekuwa na mafanikio makubwa ndani na anga za kimataifa ikiwamo kuzoa tuzo mbalimbali ikiwamo za MTV Ulaya (MTV European Music Awards, EMAs kwa mwaka 2023 akiwa Msanii Bora kutokea Afrika (Best African Act).

Tuzo hiyo aliyoipata mapema mwezi huu imemfanya awe msanii wa kwanza wa Afrika na Afrika Mashariki kushinda tuzo tatu za MTV EMAs. kwani alishinda mbili mwaka 2015. Katika muziki ameshirikiana na mastaa mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live